UONGOZI wa
Simba umesema kuwa nyota wao wote waliowasili kambini jana maeneo wamefanyiwa vipimo vyote muhimu ikiwa ni pamoja na Virusi vya Corona ili kujua
hali zao kabla ya kuanza mazoezi.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amesema kuwa wameanza mchakato
wa kuwapokea wachezaji wao ambao walianza kuwasili kambini jana.
“Utaratibu
uliopo kwa sasa ni kwa wachezaji wa ndani kuanza kuripoti kambini na kazi ya
kwanza ni kufanyiwa vipimo ikiwa ni pamoja na Corona lengo ni kujua afya zao
kabla ya kuanza mazoezi.
“Kila kitu
kinakwenda kwa program na jambo la kwanza ilikuwa kuwasili kambini kisha
kupimwa na kuwapa maelekezo ya kitaalamu namna ya kujikinga na Corona," amesema.








Mbona upande wa pili nimeona nao tayari wameanza mazoezi ila sijaona wakipimana corona kama sie,kweli simba club kubwa
ReplyDeleteKwa sababu ya mahaba uliyonayo kwa Simba huwezi upande wa pili kama nao wamefanyiwa vipimo..hilo ndilo jibu
Delete