May 25, 2020


WAZIR Jr, nyota wa Mbao FC inaelezwa kuwa amewekwa kwenye rada za Yanga ambao wanahitaji kuimarisha kikosi msimu ujao.

Habari kutoka kwa mtu wa karibu wa Jr ilieleza kuwa kumekuwa na mawasiliano baina ya meneja wa nyota huyo pamoja na uongozi wa Yanga.

"Kumekuwa na mawasiliano ya awali kati ya viongozi wa Yanga pamoja na meneja wa Jr ambapo wanahitaji kuipata saini yake baada ya kugundua kwamba mkataba wake unakaribia kuisha,".

Wazir amesema kuwa masuala yake ya usajili yapo chini ya meneja wake anaweza kuondoka iwapo mipango itakamilika.

"Nilipewa taarifa kwamba kuna ofa zaidi ya nne kwa meneja wangu hivyo iwapo mambo yatakwenda sawa ninaweza kuondoka na kupata changamoto mpya.

"Bado kwa sasa nipo ndani ya Mbao mkataba wangu haujaisha hivyo wakati ukifika wa kuweka wazi kila kitu itajulikana," amesema.

Jr ametupia mabao saba ndani ya Mbao na ana pasi mbili za mabao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic