May 12, 2020


YKIPE Gislain mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa anaomba apewe muda zaidi ndani ya klabu hiyo ili kuonyesha ujuzi wake wote.

Nyota huyo alisajiliwa akitokea Klabu ya Gor Mahia ambapo alivunja mkataba wake ili kukipiga ndani ya klabu hiyo Desemba mwaka jana.

Ameshindwa kufurukuta ndani ya Yanga ambapo amefunga bao moja ndani ya Ligi Kuu Bara ilikuwa mbele ya Singida United wakati Yanga ikishinda mabao 3-1.

Yikpe amesema:" Nataka kuondoka ndani ya Yanga nikiwa nimeweka historia na kufanya makubwa kwa ajili ya timu yangu hivyo ninahitaji nafasi.

 "Nimeshindwa kufanya makubwa kwa kuwa nilikuwa sipati nafasi nikipata nafasi pale ligi itakaporejea sitafanya makosa,".

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic