UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa unajiweka sawa kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga utakaochezwa Uwanja wa Taifa, Juni,21.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria, amesema kuwa, mipango ipo sawa kutokana na kikosi kuanza kurejea kwenye ubora wake.
“Kocha Mkuu, Aristica Cioaba ameshaanza kukinoa kikosi na wachezaji wameanza kurejea kwenye utimamu wa mwili baada ya kumalizana na Mbao FC sasa hesabu zetu ni kwa Yanga.
"Tunaamini utakuwa mchezo mgumu ila tunahitaji matokeo kwani kazi yetu ni kutoa burudani kwa mashabiki na kuonyesha uwezo wetu ndani ya uwanja“
Azam FC ipo nafasi ya pili kibindoni ina pointi 57 itamenyana na Yanga iliyo nafasi ya tatu na pointi zake 55 zote zimecheza mechi 29.
0 COMMENTS:
Post a Comment