MSHAMBULIAJI wa Yikpe Gnamien, ametumia dakika 258 uwanjani akicheza mechi za Ligi Kuu Bara baada ya kujiunga na klabu hiyo kwenye usajili wa dirisha dogo.
Mwili jumba huyo alivunja mkataba na Gor Mahia ya Kenya kabla ya kuibukia ndani ya Yanga iliyo chini ya Luc Eymael ambaye ni Kocha Mkuu.
Raia huyo wa Ivory Coast amesema kuwa hajaonyesha makali kwa kuwa hakupewa nafasi kikosi cha kwanmza anaamini akipewa nafasi atafanya makubwa zaidi.
Mchezo wake wa kwanza mbele ya Singida United alitupia bao moja kwa kichwa kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Namfua wakati Yanga ikishinda mabao 3-1.

Mechi zake hizi hapa:-Simba (29), Kagera Sugar (20), Azam FC (15), Singida (23), Mtibwa (22), Lipuli (61), Ruvu Shooting (24), Prisons (60) na Polisi Tanzania (26), Namungo (2)
0 COMMENTS:
Post a Comment