WATU 300 tu ndio wataruhusiwa kuwa uwanjani wakati za Ligi Kuu England zitarejea. Hii itajumlisha idadi ya wachezaji, benchi la ufundi, wauguzi na madaktari lakini pia baadhi ya viongozi.
Pamoja na hivyo, wahusika kadhaa watakaokuwa uwanjani na idadi ya mwisho inatakiwa watu wasizidi ni 300.
Ligi Kuu England inatarajiwa kurejea Juni 17 kwa mechi za viporo na sababu kubwa ya kufanya hivi ni kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.
Vifaa vyote vya michezo ikiwa ni pamoja na mipira, bendera vitapuliziwa dawa maalumu kwa ajili ya kinga zaidi.
Mpango mkubwa uliopo kwa sasa uliopangwa na kila timu imetaarifiwa ni kuhusu utaratibu uliopangwa ni pamoja na mikutano ya waandishi wa habari kufanyika kupitia video call kipindi ligi itakaporejea.
Watu wa VAR watakaa vyumba tofauti ili kuweka umbali kujikinga dhidi ya Virusi vya Corona.
Wachezaji 20 kwa timu moja,12 dawati la madaktari na benchi la ufundi,10 viongozi kutoka kila timu.
Hakutakuwa na mashabiki ndani ya Uwanja zaidi ya watu 300 ambao wana majukumu maalumu ya kufanya.
Watu wa uzalishaji matangazo (production manager ) hawatazidi 23 kwa upande wa waandishi watahitajika 60.
0 COMMENTS:
Post a Comment