June 16, 2020


KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison bado ni pasua kichwa kwa sasa kwani inaelezwa kuwa yupo kwenye hesabu za Simba jambo linalomfanya asiwe na timu kwa sasa kambini Dodoma.

Yanga inajiandaa na mchezo wake wa kesho, Juni 17 Uwanja wa Jamhuri utakaopigwa majira ya saa 10:00 jioni huku nyota huyo akiwa hajajiunga na timu.

Hivi karibuni Morrison alikiri kuwa amefanya mazungumzo na Simba huku akipewa kiasi cha fedha ikiwa ni njia ya kumshawishi ajiunge na watani hao wa jadi.

Habari kutoka ndani ya Yanga zinaeleza kuwa mpaka sasa hawajafanya mazungumzo yoyote na mchezaji huyo kwa kuwa wapo Dodoma wakijianda na mchezo dhidi ya JKT Tanzania.

"Mpaka sasa Yanga haijazungumza na Morrison kwani viongozi akili zao wameziweka kwenye mchezo wa kesho dhidi ya JKT Tanzania hivyo watakaa naye mezani pale watakaporejea," ilieleza taarifa hiyo.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa hakuna tatizo lililopo na mchezaji huyo ila wakirejea watajua namna ya kufanya.

Morrison aliukosa mchezo wa Mwadui FC Juni 13 na kesho ataukosa mchezo dhidi ya JKT Tanzania.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic