June 16, 2020


KIUNGO mshambuliaji wa Yanga Bernard Morrison ametua makao makuu ya Yanga ili kuzungumza masuala yanayomhusu.

Morrison hakusafiri na timu ambayo ilicheza mchezo na Mwadui FC mkoani Shinyanga kutokana na sababu ambazo alieleza kuwa hayupo fiti. 

Ilitarajiwa angejiunga na timu Dodoma kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya JKT Tanzania ila haikuwa hivyo jambo lililofanya uongozi kufanya jitihada za kuzungumza naye.

Morrison amefanya mazungumzo na Kaimu Katibu Mkuu, Adv. Simon Patrick ambaye amechukua nafasi ya David Ruhago aliyesepa madarakani jana.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic