June 4, 2020

  
INAELEZWA kuwa beki chipukizi, anayekipiga ndani ya Klabu ya Coastal Union Bakari Mwamnyeto amemalizana na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba.
Mwamnyeto sarakasi zake za usajili zilianza tangu msimu uliopita ambapo Simba na Yanga zilikuwa zinahitaji kuipata saini yake. Simba inaonekana imeipundia Yanga na kuibuka washindi.
Awali ilielezwa kuwa Yanga imemfuata beki huyo ambapo aliwaeleza njia ya kumpata ni kuzungumza na mabosi wake ambao ni Coastal Union na dau lake likitajwa kuwa ni milioni 80 jambo lililowakimbiza Yanga mezani.
Taarifa kutoka chanzo cha kuaminika zimeleza kuwa:-“Yanga ilikuwa inahitaji kumpata Mwamnyeto na ilikuwa imefanya mazungumzo na beki mwenyewe ambaye aliwaambia wazungumze na uongozi wa timu yake, kilichowakimbiza Yanga ni dau jambo ambalo Simba wamelitumia kuwa nafasi ya ushindi.
“Kwa asilimia 99, Simba imemalizana na beki huyo pamoja na Uongozi wa Coastal Union kukubali kumruhusu kuondoka baada ya kukamilisha mazungumzo ya awali na Simba kukubali kuvunja benki ili kutoa dau la milioni 80 ambalo analihitaji mchezaji huyo hivyo msimu ukiisha tu, jamaa anahamisha makazi mpaka Msimbazi.
“Mchezaji mwenyewe pia kilichomfanya akubali kutua Simba ni nafasi yake pia ya kucheza kwani ameangalia Yanga ameona kuna wachezaji wengi vijana kwenye nafasi yake ikiwa ni pamoja na Ally Mtoni na All Ally ila kwa Simba pale wengi wamemzidi umri ikiwa ni pamoja na Pascal Wawa na Erasto Nyoni ambao ni wakongwe  anaona itakuwa rahisi kuingia kwenye mfumo,” ilieleza taarifa hiyo.
Mwamnyeto ambaye pia ni nahodha ndani ya Coastal Union, ameweza kuingoza safu yake ya ulinzi kufungwa mabao machache ikiwa imecheza mechi 28 ambayo ni 19 pia naye amefunga bao moja kati ya mabao 27.
Coastal Union, ipo nafasi ya tano kwenye msimamo ikiwa na pointi zake 46 ni miongoni mwa timu zenye safu kali ya ulinzi kwa msimu wa 2019/20.
Beki huyo amesema kuwa suala la yeye kuondoka ndani ya Coastal Union inawezekana ikiwa utaratibu utafuatwa.
“Mimi ni mchezaji sichagui sehemu ya kucheza ama kuweka kambi, kikubwa utaratibu ufuatwe nami nitapiga kazi na timu ambayo imefuata utaratibu iwe Simba ama Yanga sina tatizo kabisa,” alisema. 

Chanzo:Championi

2 COMMENTS:

  1. Mwenye nguvu jamani apishwe. Yuwapi Mnyama aliewahi kumsujuduisha Simba mwenye mngurumo kama wa radi na makucha makali kuliko wembe. Cut your coat according to the cloth you have

    ReplyDelete
  2. Injinia wao kasema tusubiri kutangazwa wasafi fm

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic