June 4, 2020


MASHABIKI na wapenzi soka nchi walikuwa na hamu ya kuona tena, Ligi Kuu Bara inarejea uwanjani kwa mara nyingine, hii ni baada ya kupigwa stop kwa miezi zaidi ya miwili kutokana na janga la virusi vya Corona.
 Juni 13, masuala ya michezo kwa upande wa Ligi Kuu Bara, Ligi Daraja LA Kwanza na la Pili zitaanza kutimua vumbi katika viwanja tofauti hapa nchini hii ni baada ya Shirikisho la Soka (TFF) kwa kushirikiana na Bodi ya Ligi kuweka mambo sawa na kutangaza tarehe hiyo.
 Serikali tayari imetoa maelekezo kuhusu kurejea kwa masuala ya michezo pamoja na utaratibu ambao unapaswa ufuatwe wakati ligi itakapoendelea.
 Awali  ilikuwa soka litakaporejea lichezwe bila ya mashabiki na ilipendekezwa kuwa ligi ingeendelea lakini michezo yote ingepigwa katika vituo viwili Dar es Salaam na Mwanza.
Dar ilikuwa kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho huku Mwanza ikiwa kwa ajili ya Ligi Daraja la Kwanza na la Pili.
 Lakini kwa  sasa taarifa rasmi ya Serikali iliyotolewa hivi karibuni na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Hassan Abbas ni kwamba mashabiki ni ruksa kuingia uwanjani iwapo watahitaji ila kwa kuzingatia kanuni za afya.
Wadau wote kiujumla wa masuala ya michezo ikiwa ni pamoja na ndugu msomaji ni lazima kufuata muongozo huo ambao umetolewa na Serikali. Kwenye muongozo huo unazungumzia masuala muhimu ya kufanya kwa shabiki anayetaka kwenda uwanjani ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa.
Mbali na kuvaa barakoa pia ni lazima shabiki anawe kwa maji tiririka pamoja na kukaa umbali wa mita moja awapo uwanjani.
 Lakini tunaamini hayo maelekezo ambayo yametolewa hasa suala la mashabiki kuingia uwanjani watakiwa kuwa makini na kuzingatia masuala ya afya kwa kuchukua tahadhari dhidi ya Corona kwani bado ipo.
 Kama mashabiki wote watafuata maelekezo ya watu wa afya pindi wanapoingia uwanjani itakuwa ni jambo nzuri zaidi kwani watakuwa wanalinda afya zao na kuepuka kupata maambuziki ya Virusi vya Corona.
Inafahamika  kuwa mashabiki ni watu ambao huwa na mambo mengi hasa wakiwa ndani ya uwanja na hata nje hasa pale wanapoingia kwenda kuzishangilia  timu huwa na vituko vya hapa na pela.
 Kwa kipindi hiki ambacho kuna Virusi vya Corona ni vyema wakapunguza mihemko ili kuhakikisha tu mambo yaweze kwenda sawa katika hili.
Tunaamini kabisa kama shabiki umeamua kwenda kutazama soka na unajua hali halisi ya sasa ni vizuri ukazingatia yale ambaye ambayo yametolewa kama mwongozo na wataalumu wa afya.
Kwanza ni jambo la kipekee kwa mashabiki wa Tanzania kuweza kupata nafasi ya kwenda kuzitazama timu zao sababu nchi nyingi ligi zinaendelea lakini hakuna mashabiki  ambao wameruhusiwa kutazama ligi kutokana  na janga la Virusi vya Corona.
 Cha la msingi mashabiki muende viwanjani kwa utaratibu na kuzingatia yote, bila kwenda kinyume kwa manufaa yenu pamoja na familia zenu kwa kujinga na kuchukua tahadhari na ikumbukwe kuwa wale watakaokiuka adhabu zitawahusu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic