June 5, 2020


BODI ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TBLB) imefanya mabadiliko kwa ratiba za michezo iliyopangwa kufanyika Juni 30 na Julai Mosi za raundi ya 31 na kuzirudisha nyuma hadi Juni 27 na 28.

Mechi hizo ni za Ligi Kuu Bara, Ligi Daraja la Kwanza na la Pili ambazo zimekuwa na mabadiliko kwa sasa.

Kwa Ligi Kuu Bara itakuwa ni dhidi ya ya Mwadui v Mtibwa Sugar, ilipangwa kuchezwa Juni 30 Mbeya City v JKT Tanzania awali ilipangwa Juni 30, Mbao v Polisi Tanzania awali ilipangwa Juni 30 na Singida United v Lipuli,awali ilipangwa Juni 30 Ruvu Shooting v Namungo na awali ilipangwa Julai Mosi, Yanga v Ndanda awali ilipangwa Julai Mosi, Alliance v Coastal Union awali ilipangwa Julai Mosi Biashara United v Azam FC awali ilipangwa Julai Mosi hizi zitapigwa Juni 27.

Kwa Ligi Daraja la Kwanza ni raundi ya 19 ambayo itakuwa hivi;- African Lyon v Boma FC itachezwa Juni 19 ule wa raundi ya 20 kati ya Sahare All Stars dhidi ya Mawenzi Market itachezwa Juni 27.

Ligi Daraja la Pili:-Mpwapwa United v Villa Squad, Rufiji v Dar City, African Sports v Eagle na Mkamba Rangers v Mbuni itatapigwa Juni 28 badala ya Juni 27.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic