June 19, 2020


UONGOZI wa JKT Tanzania umesema kuwa makosa waliyoyafanya Juni 17 kwa kushindwa kufuata muongozo uliowekwa na Serikali kwa kushindwa kuweka umbali wa mita moja wanahitaji msamaha.

Kocha Mkuu wa JKT Tanzania, Abdalah Mohamed,'Bares' amesema kuwa wanahitaji msamaha wa makosa yao kwani mechi ilikuwa na ushindani mkubwa.

Mchezo huo ulikuwa kati ya JKT Tanzania na Yanga na ulikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

"Ilikuwa ni mechi ngumu na mashabiki wengi walijitokeza kuona namna gani mchezo utakuwa ila mwisho wa siku utaratibu haukkufuatwa tunaomba radhi katika hili," amesema.

JKT Tanzania imezuiwa kucheza na mashabiki kwa mechi zake zote zilizobaki za ushindani kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na mechi zao ambazo zimebaki ni pamoa na Mbao, Singida United na Alliance

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic