MKURUGENZI wa Uwekezaji GSM, Injinia Hersi Said amesema kuwa sababu kubwa ya Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael kuchelewa kurejea Bongo ni kukosa nafasi kwenye ndege.
Hivi karibuni ilielezwa kuwa Eymael hajatumiwa tiketi na uongozi wa Yanga jambo ambalo lilimfanya afanye kazi akiwa nchini Ubelgiji ambako alikwenda baada ya Serikali kusimamisha masuala ya michezo kutokana na kuibuka kwa janga la Virusi vya Corona.
Kwa sasa Serikali imeruhusu masuala ya michezo kwa kueleza kuwa hali ya maambukizi imepungua na Yanga kibarua chake cha kwanza kwenye ligi itakuwa dhidi ya Mwadui FC Juni 13, Uwanja wa Kambarage.
Said amesema kuwa:' Tiketi kocha, Luc Eymael anayo sababu alikata tiketi ya kwenda na kurudi kuchelewa kutua nchini akitokea Ubelgiji ni kutokana na kusimama kwa safari mbalimbali za ndege kufuatia janga la Virusi vya Corona.
"Mashabiki wasiwe na wasiwasi mwalimu atarudi kuendeleza majukumu yake ya kazi kwani kila kitu kinakwenda sawa na tiketi anayo hilo halina tatizo, alikosa nafasi kwenye ndege ya kwanza ambayo imetua nchini hivi karibuni baada ya ndege kuanza kupaa," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment