June 5, 2020



UONGOZI wa Klabu ya Pamba SC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza umeishukuru mamlaka ya Bodi ya Ligi Tanzania Bara,(TPLB) pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni moja kwa ajili ya kuzisaidia timu zinazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza na la Pili kumaliza msimu wa 2019/20.

Akizungumza na Saleh Jembe, Makamu Mwenyekiti wa Pamba SC, Aleem Albhai amesema kuwa ni jambo la kushukuru kwa sapoti waliyopewa ya milioni moja.

"Ninawashukuru TPLB na TFF kuwa tunapewa sapoti kwa kuwa maandalizi ya ligi yanahitaji gharama kubwa, nina amini kwamba tutafanya vizuri kwenye mechi zetu zilizobaki. 

"Tunaomba pia izidi kuyatazama maombi yetu ambayo tumeyaomba kwani ni muda mrefu kuna mambo mengi ya kufanya ili kufikia mafanikio," amesema.

Juni 20 mwaka huu Ligi Daraja la Kwanza inatarajiwa kurejea rasmi baada ya kusimama kwa zaidi ya miezi miwili kutokana na janga la Corona.

Serikali imeruhusu masuala ya michezo kuanza baada ya kusimamishwa tangu Machi 17 kutokana na janga la Virusi vya Corona.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic