June 9, 2020

KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa anatarajia kuwasili nchini Juni 10 ambayo ni Jumatano baada ya kutumiwa tiketi ya ndege na uongozi wa Yanga.
Eymael raia wa Ubelgiji alisepa Bongo baada ya Serikali kusimamisha masuala ya michezo Machi 17 ambapo ilielezwa kuwa mbali na mapumziko hayo alikuwa na mpango wa kwenda kuoa.
Kwa sasa tayari Serikali imeruhusu masuala ya michezo kuendelea kwa kueleza kuwa hali ya maambukizi ya Corona imepungua. Tayari Yanga ilianza mazoezi tangu Mei 27 ikiwa chini ya Kocha Msaidizi Charlse Mkwassa.
Awali Eymael alinukuliwa akilalamika kuwa hajatumiwa tiketi ya ndege jamb ambalo lilimfanya afanye kazi akiwa Ubelgiji kwa tabu.
 Eymael amesema kuwa alishindwa kuthibitisha mapema safari ya kurejea kwake nchini Juni 7 kwa kudhani kwamba waliopaswa wadhibitishe safari yao walikuwa ni Yanga.
“Nilipaswa kurejea nchini Juni 7 ila nilishindwa kwa kuwa sikuthibitisha uwepo wangu kwenye kampuni ya ndege nilidhani kwamba wanaopaswa kufanya hivyo ni Yanga, ila tayari nimeshapata tiketi na ninatarajia kurejea nchini Jumatano,” alisema Eymael.

Iwapo atatua mapema Juni 10 ana uhakika wa kuwahi mchezo wa Ligi Kuu Bara ambapo Yanga itamenyana na Mwadui FC, Juni 14 Uwanja wa Kambarage.

Chanzo:Championi


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic