JUMA Abdul, nahodha msaidizi wa Klabu ya Yanga, amesema kuwa Kocha Mkuu, Luc Eymael aliwaambia wachezaji kwamba atakayeongezeka uzito atakatwa mshahara wake ikiwa ni sehemu ya adhabu.
Abdul amesema kuwa Eymael aliwapa programu maalumu za kufanya kwa ajili ya kulinda vipaji vyao wakati wa mapumziko yaliyosababishwa na janga la Corona na kutoa onyo kwa wachezaji wote.
“Kocha alisema kuwa mchezaji ambaye ataongezeka uzito, huyo lazima atakatwa mshahara, ninaamini atakapopewa ripoti kazi ya kwanza itakuwa ni kutazama wale ambao wameshindwa kutimiza vigezo vyake,” alisema Abdul.
Inaelezwa kuwa walioongezeka uzito ambao panga la mshahara linawasubiri ni pamoja na David Molinga, Patrick Sibomana na Abdulaziz Makame
Morrison nae pia kaingia mitini hakuwepo ndani ya basi na majaribio ya kumtafuta hayakufuwa dafu
ReplyDeleteMorisson ni staa Leo watampandisha ndege. Hali inaleta mgawanyiko baina ya wachezaji.Acheni kuwagawa wachezaji nyie viongozi.Wanachama hatupendi hali hii itokee.Itaathiri moral ya wachezaji.
ReplyDelete