MAJEMBE ya kazi yanayokipiga ndani ya kikosi cha Azam FC yameanza kushuka Bongo taratibu.
Leo Juni 15, wachezaji wawili kutoka Zimbabwe, beki wa kushoto, Bruce Kangwa na kiungo mshambuliaji, Never Tigere wametua rasmi Bongo.
Wachezaji hao walikwama nchini kwao Zimbabwe kutokana na vikwazo vya ugonjwa wa Virusi vya Corona, lakini jitihada za uongozi wa Azam FC zimefanikisha wawili hao kuwasili nchini.
Wachezaji pekee ambao bado hawajawasili nchini kuungana na wenzao kumalizia mechi za ligi na Kombe la FA (ASFC), ni Waghana, kipa Razack Abalora, mabeki wa kati, Daniel Amoah na Yakubu Mohammed.
Kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho ikiwa ni hatua ya Robo Fainali, Azam FC inatarajiwa kumenyana na Simba, Julai 30 Uwanja wa Taifa.

KwaniAzam ina mechi na Simba peke yaje?
ReplyDeleteWamekuja kwaajili ya kucheza mech na simba basi mech ikiisha waludi kwao
ReplyDelete