JUMA Abdul nahodha msaidizi ni kinara wa kumwaga maji ndani ya klabu ya Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu, Luc Eymael raia wa Ubelgiji.
Yanga ikiwa imefunga mabao 31 baada ya kucheza mechi 27 ametoa jumla ya pasi tano za mabao ambapo mbili katika hizo zilikutana na kiungo mshambuliaji Bernard Morrison.
Katika pasi zake zote alizotoa kwa msimu huu ametumia zaidi mguu wa kulia ambapo amesema kuwa sababu kubwa ya kutumia mguu huo ni kukutana na mipira mingi yenye nguvu upande wake wa kulia.
Papy Tshishimbi, ambaye ni nahodha ametoa pasi moja ya bao ilikuwa mbele ya Biashara United wakati Yanga ikishinda kwa bao 1-0.
Abdul ameongeza kuwa yote yanayotokea uwanjani ni kazi kubwa ambayo inafanywa kwa ushirikiano jambo ambalo linawapa matokeo chanya.
0 COMMENTS:
Post a Comment