SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amevurugwa na dakika 624 za kiungo wake mshambuliaji, Luis Miqussone kwa kufanya mambo makubwa uwanjani licha ya kutumia muda kiduchu.
Miqussone ni ingizo jipya ndani ya Simba lilitua kwenye usajili wa dirisha dogo akitokea UD Songo amekuwa kipenzi cha mashabiki kutokana na usajili wake kujibu haraka.
Sven amesema kuwa kiungo huyo ni miongoni mwa wachezaji muhimu kikosini kwake kwani amekuwa na mchango mkubwa licha ya kuwa na muda mfupi.
“Ninaona ni aina ya mchezaji ambaye ana vitu vingi akiwa uwanjani, namna anavyoonesha jitihada ndani ya uwanja kwa kutafuta nafasi za kufunga ama kutengeneza ni mambo ambayo yanahitajika kwa kila mchezaji, licha ya kuwa na muda mfupi bado ana onekana ana vitu vingi,” alisema.
Miqussone ametumia dakika 624 uwanjani akicheza mechi nane kwenye mabao 63 ya Simba amehusika katika mabao manne ambapo amefunga matatu na kutoa pasi moja ya bao.
Hizi hapa mechi zake:-JKT Tanzania (90), Mtibwa Sugar (16), Kagera Sugar (90), Biashara United (90), KMC (75) na Azam (83), Yanga (90), Singida United (90)
0 COMMENTS:
Post a Comment