June 4, 2020



JUNI 13 masuala ya michezo yanarejea baada ya Serikali kuruhusu burudani kuendelea baada ya kusimama kutokana na janga la Virusi vya Corona.
Nikukumbushe kwamba tangu Machi 17 hakukuwa na mechi yoyote ya ushindani ambayo iliendelea kuchezwa ndani ya uwanja.
Kikubwa ilikuwa ni kutokana na janga la Virusi vya Corona ambavyo bado vinawasumbua wataalamu kutafuta dawa ya kutibu janga hili ambalo linaivuruga dunia.
 Serikali ilisimamisha shughuli za mpira kutokana na janga la Virusi vya Corona ambalo limeivuruga dunia hivyo ilikuwa ni muhimu kwa ajili ya kuchukua tahadhari.
Maisha yalikuwa tofauti yake kwani kukosa burudani ya mpira ilikuwa ni ngumu kwa mashabiki na wanafamilia ya michezo kuweza kuiweka akilini hali hiyo.
Hakukuwa na chaguo kwani janga la Corona lilikuwa linaitikisa dunia na ili kujilinda ilikuwa lazima kuchukua tahadhari kwa kupambana na Corona kwanza huku tahadhari ili maisha yaendelee.
 Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli, amesema kuwa hali ya maambukizi ya Corona imepungua na ni muhimu kuchukua tahadhari licha ya kwamba masuala ya michezo yameruhusiwa.
Kitu kikubwa ambacho Serikali imesema kuwa ni muhimu sana kufuata muongozo ambao umewekwa ili kila timu iwalinde mashabiki wake pamoja na afya za wachezaji.
Kwa hatua ambayo Serikali imeamua kufanya inapaswa ipongezwa kwani imerejesha burudani kwa familia ya michezo na kuona namna gani burudani itaendelea.
 Kikubwa ambacho kinatakiwa kufanyika kwa sasa ni kuendelea kuchukua tahadhari na kufuata yale maagizo ambayo yametolewa kwa wadau.
Jambo la msingi kuhusu afya yetu ni kuona kwamba kitu kitakachotufanya tuendelee kuwa salama ni kuchukua tahadhari wakati wote bila kujali maambukizi yamepungua haina maana kwamba Corona imeisha.
Kazi ambayo ipo mikononi mwa viongozi wa timu zote pamoja na wadau ni kuufuata muongozo ambao umetolewa kwa wadau wote bila kujali yeye ni nani.
Tunatambua kuwa mamlaka ya Serikali imekuwa ikitupa taarifa kwamba hali imeanza kuwa shwari lakini bado wanatusisitiza tuchukue tahadhari kwani bado janga halijaisha.
Ulimwengu wa soka ambao ulikaa kimya tangu Machi 17 sasa Juni13 mambo yatakuwa hadharani na burudani itaendelea pale ilipoishia.
Muda mrefu umepita sasa bila kushuhudia burudani ya soka uwanjani na kwa sasa tunahesabu siku tu ili kuona namna gani kazi ndani ya uwanja itakuwa.
 Kwa muda huu ambao tunapitia tusijisahau na tukadhani labda mambo yamekwisha na kuendelea kuishi maisha tuliyoyazoea tahadhari ni lazima iendelee kuchukuliwa.
Tahadhari zinazotakiwa kuchukuliwa hapa ni zile ambazo kila siku zinatolewa na Serikali yenyewe kupitia Wizara ya afya pamoja na wataalamu kuhusu utaratibu unaotakiwa kufanyika kwa wakati huu.
Hapa tunakumbushana kwani afya ni muhumu ndugu yangu msomaji ndio maana leo tunaendelea kuwa wazima kwa kuwa tuna utajiri wa afya ambayo tumepewa na Mungu.
Ukweli ni kwamba iwapo mtu yoyote atakuwa anafanya kinyume na utaratibu ili awe salama kwa kupuuzia ni rahisi kutokuwa salama.
Tusisahau kwamba kwa sasa tayari Serikali pia imeruhusu kila shabiki anayependa kwenda uwanjani lazima afike iwapo atakuwa na utayari wa kwenda uwanjani.
Kikubwa ambacho wengi walikuwa wanasubiri ni kuona idadi ya mashabiki 10 iliyotolewa awali ingeendelea ila kutokana na Serikali kuona kwamba hali imeanza kuwa shwari kwa upande wa maambukizi.
Timu zilizokuwa zinatazama mapato na kuvimbisha akaunti zao  kwa sasa mambo yamewarudia kutokana na hilo lipo wazi  ni muhimu kutambua kwamba kazi kubwa ya kila timu ni kulinda usalama wa mashabiki.
Pia isitoshe kusema kwamba kwa sasa mechi ambazo zimebaki ni chache hazizidi 12 kwa timu zote ndani ya ligi hivyo ni muhimu kuangalia utajiri wa mashabiki wa kesho kuliko kuwatumia kwa sasa.
Ninarudia tena kwamba afya za mashabiki ni muhimu hivyo ni lazima ule muongozo uliotolewa na Serikali unafuatwa bila kupinga kwa kuwa atakayekiuka atapewa adhabu.
Wizara ya afya pamoja na Serikali inajali afya za watu na inatambua kwamba nguvu kazi za watu zinategemea afya bora ambayo ni muhimu kulindwa kwa sasa.
Kwenye mpango wa kurejea ligi pia ni afya pia inahitajika kwani wachezaji hawawezi kucheza iwapo hawatakuwa na afya bora hata mashabiki hawataweza kushangilia iwapo hatakuwa na afya.
Utaratibu upo wazi kwa sasa kwamba lazima wenyeji waandae vifaa maalumu ambavyo vitatumika kwa ajili ya kujilinda dhidi ya Virusi vya Corona.
Mashabiki ambao wataingia uwanjani wasisahau kwamba ni lazima kila mmoja kuwa na kifaa chake cha kujilinda ili kuwa salama kwanza kwani afya ni muhimu.
Kuvaa barakoa kwa kila shabiki atakayekuwa anahitaji kwenda uwanjani ni muhimu kwani lile zuio la mashabiki 10 limefutwa na Serikali imeridhia maisha yaendelee kama kawaida.
Corona ipo tusijidanganye kwamba vita imekwisha hapana ni muhimu kuchukua tahadhari hivyo kwa upande wa mashabiki timu zinapaswa ziangaliwe.
Tusisahau kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Corona ndugu zangu hili janga bado tupo nalo ni muhimu kujilinda kwa kuchukua tahadhari na kufuata kanuni za afya.
Tayari imewekwa wazi kuwa ni lazima kila mmoja anakazi ya kuchukua tahadhari yeye pamoja na jamii inayomzunguka ili abaki kuwa salama.
Lazima mashabiki wasijisahau pale watakapoingia uwanjani kunawa mikono kwa maji tiririka ikiwa ni mwendelezo wa kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.
Muhimu afya kuwa salama ili wakati ujao vita hii ya Corona itakapokwisha nawe pia uwe ndani ya uwanja ukicheka kwa kuwa umemshinda adui.
Maadalizi pia ni muhimu kwa sasa kwa timu ambazo zinakabiliwa na anguko la kushuka daraja zisijisahau zikadhani vita imekwisha.
Kikubwa wakati tunapambania afya zetu tukumbuke pia kupambania nafasi zetu ndani ya ligi ili pale mambo yatakapokuwa sawa ushindani uendelee.
Kwa sasa Juni 13 sio mbali na tayari muda unazidi kumeguka taratibu na ratiba ipo wazi kwani kila mmoja anajua atakutana na nani kwenye mchezo wake.
Kila mmoja ana kazi ya kufanya kujlinda na kuamua ni namna gani anaweza kujitoa na kupambana katika kufikia malengo ambayo amejiwekea kwani mashabiki ni muhimu kuona wanapata furaha huku wakiwa na malengo ya kufikia kile wanachokisubiri.
Ninaamini kwa sasa muda ambao wamepewa utatosha kujiandaa kwani nina imani wachezaji walipewa program za kufanya ili kulinda vipaji.
Muda wa kuona burudani upo njiani hivyo ni muhimu kujiweka sawa na kujipanga kuendelea pale ambapo kazi ilikuwa imeishia wakati ule ligi inasimamishwa.
Ninaamini wengi wameanza kubadilika kwa kuchukua tahadhari na kufanya yale ambayo yanashauriwa na wataalamu wetu wa afya pamoja na Serikali kiujumla.

Wizara ya afya na Serikali katika hili pia wanastahili pongezi kwani taarifa zimekuwa zikitolewa mara kwa mara kuhusu namna ya kujilinda na Corona.
Kanuni ni zilezile hazibadiliki kunawa mikono, umbali wa mita moja, kuvaa barakoa  ila kitu cha msingi hapa ni namna ya kuzifuata na kufanya kile ambacho kinaelekezwa na wataalamu wetu.
Unapozungumzia afya ni utajiri mkubwa ambao kila mmoja anapaswa kupambana kuwa salama yeye na wale ambao wanamzunguka kwa wakati uliopo kwa sasa.
Kwa wachezaji pamoja na viongozi pia ni muhimu kuendelea kuzifuata kanuni zile za afya ili kuendelea kuwa salama kwa wakati huu mgumu.
Muhimu kukumbuka kwamba kila mmoja ana kazi ya kujilinda huku muongozo ukiweka wazi kwamba kila mmoja kazi ya msingi inakuwa ni kutafuta ushindi na kuchukua tahadhari.
Nina amini vita itakuwa kali hasa baada ya ligi kurejea kutokana na kila timu kupanga kufanya vizuri kwa mechi za mwisho ambazo zimebaki kwani kila mmoja anahitaji ushindi.
Tunatarajia kutakuwa na ushindani mkubwa kwa kila timu kuonyesha kwamba ilikuwa inastahili kupata matokeo mazuri yatakayowafikisha kwenye malengo yao.
Kazi kwa timu ambazo zipo kwenye hatari ya kushuka daraja zinapaswa zikazane kujiokoa ili msimu ujao ziwe ndani ya ligi.
Jambo la kuzingatia mamlaka husika za soka ikiwa ni TFF kuanza kuangalia ni namna gani mambo yanaweza kwenda sawa na kutoa taarifa kwa wakati ili timu zijiweke sawa.
Muda huu wa maandalizi ni lazima kila mmoja kuchukua tahadhari na kufanya kazi kubwa ya kujilinda dhidi ya Virusi vya Corona ambavyo bado vipo.
Zile zinazojipanga kupanda daraja ni lazima zitazame namna zitakavyoweza kwenda kwa kasi kwenye ligi iwapo zitapanda.
Jambo la msingi kwa sasa ni kila mmoja kuchukua tahadhari na kuamini kwamba ugonjwa upo na ligi ipo tunatarajia kuona burudani.
Napenda kuwaomba kwamba kwa wakati huu kila mmoja awe balozi mzuri kwenye mapambano haya na tukishinda tushinde pamoja vita hii ambayo inasumbua vichwa vya wengi.
Muda wa maandalizi ambao umetolewa pia nao unapaswa utumike kwa umakini na tahadari ili kuendelea kulinda afya za wachezaji kabla ligi haijarejea.
Viongozi wa Ligi Kuu Bara, Ligi Daraja la Kwanza na la Pili ni lazima kuja na mkakati wa muda mfupi utakaotumika kumaliza mechi ambazo zimebaki huku wakifuata muongozo ambao umetolewa.
Timu ambazo zinashuka ni nyingi hivyo vita itakuwa ni kubwa ndani ya uwanja kwenye kutafuta matokeo na hicho ndicho kinatakiwa.
Tuna kazi kubwa ya kushinda vita hii ya Corona inayovurugavuruga kila masuala kwa sasa inatosha kusema kwamba tuendelee kuchukua tahadhari ili kuwa salama.
Itatusaidia kuturejesha kwenye njia ambayo tulikuwepo awali wakati ule wa kushuhudia zile burudani ndani ya uwanja na tusipuuzie maagizo ambayo tunapewa.
Kikubwa kwa timu kuwa tayari kupambana ndani ya uwanja kutafuta matokeo chanya ambayo ni muhimu kwa kila mchezaji na timu kiujumla.
Ukweli ni kwamba Corona ipo hata Serikali yenyewe imesema lakini cha muhimu ni lazima kuchukua tahadhari.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic