UONGOZI wa kampuni ya GSM umesema kuwa uliamua kusajili wachezaji ndani ya Klabu ya Yanga ili kuboresha kikosi na kuongeza ushindani.
Injinia, Hersi Said amesema kuwa waliamua kutumia gharama zao wenyewe kusajili nyota wanne ambao wamekuwa na mchango mkubwa ndani ya kikoi cha Yanga.
"Tulifanya usajili wa wachezaji kwa gharama zetu GSM ambao ni Ditram Nchimbi, Haruna Niyonzima, Adeyum Saleh na Benard Morisson lengo lilikuwa ni kuboresha kikosi," amesema.
Nyota hawa wamehusika kwenye jumla ya mabao nane kati ya 31 ambayo yamefungwa na Yanga ndani ya Ligi Kuu Bara.
Morrison ametupia mabao matatu, Nchimbi na Adeyum wametupia mabao mawili ndani ya Yanga huku Niyonzima akiwa na bao moja.
0 COMMENTS:
Post a Comment