NAHODHA wa Simba, John Bocco amesema kuwa wanahitaji kubeba mataji makubwa mawili ili kufikia malengo ambayo wameyapanga.
Bocco ametaja makombe hayo kuwa ni Kombe la Shirikisho lililo chini ya Azam FC pamoja na Ligi Kuu Bara ambalo lipo mkononi mwao kwa sasa, ikiwa wataweza kulitwaa na hili watakuwa wamebeba taji hilo mara tatu mfululizo.
Simba imeshaanza mazoezi yake ya kujiweka sawa ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck tangu Mei 27 na mchezo wao wa kwanza utakuwa dhidi ya Ruvu Shooting Juni 14 Uwanja wa Taifa.
Bocco amesema:"Tumeanza mazoezi na tunazidi kuwa imara kadri siku zinavyokwenda hilo ni jambo jema kwetu, kikubwa ni kuona kwamba tunafikia malengo yetu kwa kutwaa taji la Kombe la Shirikisho pamoja na ligi.
"Yote yanawezekana kwa kuwa kila mchezaji ana morali kubwa ya kutafuta mafanikio na mazoezi ambayo tumeyaanza tunazidi kuwa imara kila siku kikubwa ni sapoti ya mashabiki ili kuona yale tuliyopanga yanakamilika," amesema.
Hakukuwa na mechi ya ushindani tangu Machi 17 kutokana na janga la Virusi vya Corona ila kwa sasa Serikali imeruhusu masuala ya michezo, Juni 13 ligi itaanza rasmi kutimua vumbi.

0 COMMENTS:
Post a Comment