NAHODHA wa Yanga, Papy Tshishimbi amesema kuwa wachezaji wengi wanamkubali Kelvin Yondan kutokana na aina ya maisha ambayo anayaishi ndani ya timu.
Tshishimbi amesema kuwa ni ngumu kwa mchezaji atakayekuwa ndani ya kikosi hicho kushindwa kuendan a na falsafa ya Yondani kutokana na namna anavyobadilikabadilika.
"Kwa Yanga, Yondani ni mchezaji ambaye ni ngumu kuona anashindwa kuelewana na wachezaji wenzake na sababu kubwa ni aina ya maisha ambayo ameyachagua.
"Hapendi kuzungumza mara nyingi lakini anaweza kuishi maisha ya aina yote ikiwa ni kwa ukali anajua, upole anaweza ucheshi sasa kwa mtindo huu wa maisha anaokwenda nao ni ngumu kuona kwamba unamchukia hiyo haiwekezekani.
"Wachezaji wote wa Yanga tunaishi kwa kushirikiana na kila mmoja anapenda kufanya vile ambavyo mwenzake anapenda jambo ambalo linatufanya tuzidi kuwa na umoja," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment