KOCHA Mkuu wa Namungo FC, Hitimana Thiery, amesema kuwa hesabu zake kubwa kwa sasa ni kupata matokeo chanya kwenye mechi zake zilizobaki za Ligi Kuu Bara huku akiweka kando masuala ya usajili.
Akizungumza na Saleh Jembe, Hitimana amesema kuwa anaami kwa sasa akili zake ni lazima aziwekeze kwenye ligi kabla ya kuwaza usajili wa wachezaji.
"Kipaumbele changu kikubwa kwa sasa ni kwenye mechi za ligi kabla ya kufkikiria masuala ya usajili kwani wakati wake bado na ukifika ndipo nitajua nifanye nini.
"Tulikuwa nje kwa muda mrefu kutokana na janga la Virusi vya Corona hivyo muda huu nina kazi ya kujenga ubora na utimamu kwa wachezaji kwani tusipojipanga vema itakuwa ngumu kufikia malengo yetu," amesema.
Miongoni mwa wachezaji ambao wanatajwa kuingia kwenye rada za Namungo ni pamoja na Gerald Mdamu, mshambuliaji wa Mwadui mwenye mabao matano na pasi tatu za mabao.
Juni 13, Namungo itamenyana na Coastal Union kwenye mchezo wa ligi utakaopigwa Mkwakwani, Tanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment