MEJA mstaafu, Abdul Mingange, Kocha Mkuu wa Ndanda FC amesema kuwa mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Namungo utawarejesha kwenye ramani.
Ndanda ina kibarua kizito cha kumenyana na Biashara United Juni 20 hivyo kwa sasa inatafuta kasi ilipo kurejea kwenye ubora.
Juni Mosi, Ndanda ilirejea rasmi mazoezini baada ya Serikali kuruhusu masuala ya michezo baada ya kusimamishwa tangu Machi 17 kutokana na janga la Virusi vya Corona.
"Mechi yetu dhidi ya Namungo itatusaidia kurejea kwenye ile kasi ambayo tulikuwa nayo awali, nina amini tutaendelea pale tulipoishia kikubwa sapoti," amesema.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Juni 6 Uwanja wa Nangwanda Sijaona na kiingilio ni buku mbili.
0 COMMENTS:
Post a Comment