June 4, 2020


MOHAMED Hussein, 'Tshabalala' nahodha msaidizi wa Simba amesema kuwa wamejipanga kuendelea na balaa lao uwanjani kwenye mechi zao zilizobaki ndani ya msimu wa 2019/20.

Hakukuwa na mechi ya ushindani iliyochezwa tangu Machi 17 baada ya Serikali kusimamisha masuala ya michezo kutokana na janga la Virusi vya Corona.

Wakati Ligi Kuu Bara inasimamishwa, Simba ilikuwa nafasi ya kwanza na pointi 71, mchezo wake wa mwisho ilikuwa mbele ya Singida United ambapo ilishinda mabao 8-0.

Tayari Serikali imeruhusu masuala ya michezo kuendelea, tangu Juni Mosi kwa kueleza kuwa hali ya maambukizi imepungua na kuwataka wadau wasisahau kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona kwani bado vipo.

Tshabalala amesema:"Tulisimama tukiwa katika nafasi nzuri na mwenendo wetu haukuwa mbaya hivyo tumejipanga kuendelea pale ambapo tulikuwa tumeishia kwani hilo linawezekana na uwezo tunao. 


"Kikubwa ni kupambana kwa hali na mali ili kufikia malengo ambayo tumejiwekea, mashabiki pia waendelee kutupa sapoti," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic