June 28, 2020


SARE ya Tanzania Prisons ya bila kufungana na Simba leo Uwanja wa Sokoine Mbeya zimehalalisha rasmi ubingwa wa Simba.

Mchezo huo uliokuwa na ushindani kila timu ilikuwa ikipambana kusaka ushindi ila mwisho wa siku mbinu zikatoshana na kuwafanya wagawane pointi mojamoja.

Simba inafikisha pointi 79 ambazo haziwezi timu yoyote kwa sasa.

Wapinzani wake wakubwa ambao ni Yanga kwa sasa ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 60 baada ya kucheza mechi 32.

Mechi zake sita zilizobaki ikiwa itashinda zote itafikisha jumla ya pointi pointi 78 ambazo zimeshapotwa na Simba huku Azam ikishinda mechi zote inafikisha pointi 77.

Huu unakuwa ni ubingwa wa 21 kwa Simba na wa tatu mfululizo kubeba kwa msimu huu ilianza msimu wa 2017/18,2018/19 na 2018/20.

Kikosi cha leo cha Simba kilikuwa na mabadiliko makubwa ambapo wachezaji wengi waliokuwa hawapati nafasi kikosi cha kwanza walianza.

Prisons iliyo chini ya Kocha Mkuu, Adolf Rishard ilikuwa imara kwenye mashambulizi huku kiraka Salum Kimenya akiwa ni mwiba wa safu ya ulinzi ya Simba.

Manula alifanya kazi ya ziada kipindi cha kwanza kuikoa michomo ya Kimenya ambaye alikuwa akifanya majukumu yake ndani ya uwanja.

Baada ya sare hiyo Tanzania Prisons inafikisha jumla ya pointi 43 kibindoni.

1 COMMENTS:

  1. Hata kuandika Simba inawashinda. SASA mabingwa wa sasa ndio nini?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic