SIMBA leo imeendelea na mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho kwenye uwanja wao uliopo maeneo ya Bunju.
Juni 14 Klabu ya Simba itakuwa na kibarua cha kumenyana na Ruvu Shooting kwenye mchezo wa ligi utakaopigwa Uwanja wa Taifa.
Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa wachezaji wake wanazidi kuwa imara taratibu kwa kuwa hawakuwa na mazozi ya pamoja kwa muda mrefu.
"Hatukuwa na mazoezi ya pamoja kwa muda mrefu jambo ambalo limenifanya nianze na program hatua kwa hatua mpaka tulipo kwa sasa sio mbaya kwani kuna maendeleo ambayo ninayaona kwa wachezaji," amesema.
Ikiwa imecheza mechi 28 imejikusanyia pointi 71 kibindoni na imefunga jumla ya mabao 63.
0 COMMENTS:
Post a Comment