UONGOZI wa Yanga umesema kuwa hesabu kubwa ni kuona inaanza vema kwenye mechi za ligi ili kujenga hali ya kujiamini mwanzo mpaka mwisho wa ligi.
Yanga imecheza mechi 27 za ligi kibindoni ina pointi 51 zinazoifanya iwe nafasi ya tatu kwenye msimamo, Juni 13 itakuwa na kibarua cha kumenyana na Mwadui FC kwenye Uwanja wa Kambarage.
Antonio Nugaz, Ofisa Uhamasishaji na Msemaji wa Yanga amesema kuwa wanaamini kila kitu kinawezekana kwa kuwa wamejipanga kiukamilifu.
Tayari wachezaji wa Yanga wote wamesharipoti kambini ikiwa ni pamoja na kipa namba moja Farouk Shikalo ambaye alichelewa kujiunga na wenzake ambao walianza mazoezi Mei 27 kutokana na mipaka ya Kenya kufungwa sababu ya janga la Virusi vya Corona.
Yanga inafanyia mazoezi yake katika Uwanja wa Chuo cha Sheria, Ubungo.
0 COMMENTS:
Post a Comment