MASHABIKI wa Yanga wametisha baada ya kukomba shilingi laki mbili kutoka katika droo ya tatu ya Jishindie Gari na Championi ambayo imefanyika leo Ijumaa katika Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza Mori, Dar.
Mashabiki hao wa Yanga ambao walijitambulisha wenyewe baada ya kupigiwa simu ni Jumanne Shaban wa Manzese Dar, Mhando M. Mhano wa Tanga, Andrew Mbaya wa Dar na Amos J Paul wa Dar wao walijinasibu wazi kuwa wao ni mashabiki wa damu wa Klabu ya Yanga.
Washindi wengine ni Fadhil Salum na Tanzan Shams wote wametokea Dar na wote watazawadia shilingi 50,000 kwa kila mmoja pamoja na tisheti zenye nembo ya Bahati nasibu hiyo.
Mchakato wa kuchezesha droo uliendeshwa na Idara ya Masoko na Usambazaji chini ya Anthony Adam, Songolo Bilali, Jimmy Haroub na Memorise Richard ambaye alikuwa anasoma majina ya washindi hao na kuwapa taarifa kwa kuwapigia simu.
Bila kusahau uwepo wa mwakilishi kutoka katika Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Elibariki Sengasenga ambaye alikuja kushuhudia sheria na utaratibu wa kuchezesaha bahati basibu hiyo unafuatwa.
Mkuu wa kitengo cha usambazaji Anthony Adam amesema kuwa washindi wote wamepewa utaratibu wa namna gani watapewa zawadi zao, ambapo zoezi hilo litafanyika kuanzia Jumatatu ijayo kwa kuwa wikiendi hii itakuwa ni nafasi yao ya kuandaa zawadi hizo.
“Tumecheza droo yetu ya tatu leo Ijumaa na tumefanikiwa kupata washindi sita ambao wote watajishindia fedha shilingi 50,000 kila mmoja pamoja na tisheti zenye nembo ya bahati nasibu hiyo.
Namna ya kushiriki bahati na sibu ya kujishindia gari Adam amesema kuwa ni rahisi:"Msomaji anunee gazeti la Championi ama SpotiXtra ukurasa wa pili kuna kuponi yenye maelezo ambapo ukijaza unaweza kumpa wakala ama ukatuma kwa sanduku la posta.
"Kuponi zte zilizochezwa kwenye droo zote tatu zitachezwa pia kwenye droo kubwa ya Jishindie gari," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment