June 5, 2020


CHARLES Mkwassa, Kocha Msaidizi wa Yanga amesema kuwa wachezaji wote wameanza kurejea kwenye ubora wao huku wale ambao wameongezeka uzito wakiandaliwa program maalamu.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mkwassa amesema kuwa mechi yao ya kirafiki dhidi ya Transit Camp imewapa somo la kujua wapi walikosea ili wajipange wakati ujao. 


"Kuna wachezaji watatu ambao wameongezeka uzito hao tutawapa program maalumu ambayo itawafanya wawe bora na kurejea Kwenye ushindani.

 "Jumapili dhidi ya KMC utakuwa ni mchezo wetu wa kirafiki wa mwisho kwani muda hautaturuhusu na ratiba kwetu za ligi zitaanza, kikubwa mashabiki waendelee kutupa sapoti, pia wasisahau kwamba kuna ugonjwa wa Corona lazima wachukue tahadhari na kufuata utaratibu ambao umewekwa na Serikali pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania" amesema.

Yanga ilianza mazoezi yake Mei 27 Uwanja wa Chuo cha Sheria Ubungo ikiwa ni maandalizi kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic