AMIS Tambwe, mshambuliaji wa zamani wa Klabu ya Yanga amesema kuwa miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa bora alipokuwa akicheza nao ni pamoja na Deus Kaseke ambaye ni kiungo.
Tambwe aliachana na Yanga msimu uliopita kwa kile ambacho ilielezwa kuwa amechuja jambo ambalo amekuwa akilikanusha muda wote anaamini uwezo wake haujachuja ndio maana aliweza kufunga mabao 12.
Akizungumza na Saleh Jembe, Tambwe amesema kuwa miongoni wa wachezaji ambao anaamini ni bora ndani ya Yanga wapo wengi ikiwa ni pamoja na Kaseke kutokana na uwezo wake wa kutengeneza nafasi.
“Ninaamini kwamba wachezaji wengi ambao nilicheza nao ni bora ila sitaweza kumuacha Kaseke kwani yupo vizuri kwenye kutengeneza nafasi na kumiliki mpira ni kitu ambacho nilikuwa ninakipenda kwake.
“Ukitaka nikutajie wengine ambao nimecheza nao nitakwambia Simon Msuva, Juma Abdul, Haruna Niyonzima, Thaban Kamusoko na Papy Tshishimbi,” amesema Tambwe.
Kaseke amehusika kwenye jumla ya mabao matatu ndani ya Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu, Luc Eymael ikiwa imefunga mabao 31.
Jitafutie timu nyengine. Usijidhalilishe Ni wazi Yanga Hawana haja nawe
ReplyDelete