June 3, 2020


AZAM FC imeendelea na mazoezi yake leo ikiwa ni kujiaanda na mchezo wao wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex, Juni 14.

Kikosi hicho kitashuka uwanjani kikiwa na kumbukumbu ya kusepa na pointi tatu kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza kwa ushindi wa bao 1-0.

Utakuwa ni mchezo wa kwanza kwa Azam FC iliyo chini ya Arstica Cioaba kwa msimu huu baada ya masuala ya michezo kurejea Bongo.

Masuala ya michezo yalisimamishwa tangu Machi 17 na Serikali kutokana na janga la Virusi vya Corona na kwa sasa tayari Serikali imeruhusu shughuli za michezo kuendelea kwa kueleza kuwa hali ya maambukizi imepungua.

Mchezo huo utachezwa majira ya saa 1:00 usiku.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic