TUISILA Kisinda, winga anayekipiga AS Vita ya Congo amesea kuwa muda wowote kuanzia leo anaweza kutua Yanga.
Hivi karibuni, Yanga chini ya Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM, Injinia, Hersi Said alisema wapo katika mkakati wa kusajili winga machachari huku Kisinda akitajwa kutua Yanga.
Winga huyo amesema wapo kwenye hatua nzuri ya kumalizana na Yanga, anachosubiri ni kuja kutia saini na kuwa mchezaji halali wa timu hiyo.
“Nipo kwenye mazungumzo na Yanga kwa muda mrefu sana na katika mazungumzo ambayo tumeongea, bado hatujamalizana. Nilitakiwa nitue Dar siku nyingi huko nyuma, lakini kuna vitu havikukaa sawa. Ikashindikana.
“Kwa sasa nasubiri kutumiwa fedha ambazo tulikubaliana ili nije huko, na kama nitatumiwa wiki hii basi wiki ijayo nitatua Dar kwa ajili ya kumalizana na Yanga,” alisema winga huyo.
Alipoulizwa Hersi juu ya ujio wa nyota huyo, alisema: “Kwa sasa tupo kwenye mipango ya kuhakikisha timu inafanya vizuri katika michezo ya ligi kuu, masuala ya usajili tusiyazungumzie kwanza ila baadaye kila kitu kitakuwa wazi kwa sababu tunataka kutengeneza timu ya ushindani zaidi.”
Ikumbukwe kuwa, wadhamini wa Yanga, Kampuni ya GSM, imekuwa ikipambana kuhakikisha timu hiyo inasajili wachezaji wazuri wa kuibeba timu katika michuano mbalimbali.
Chanzo: Spoti Xtra
Tangia mmeanza kundika kuhusu wachezaji ambao wanatuwa yanga hadi sasa wameshafika 100 na bado mnaendelea hadi usajiri ukianza rasmi watakuwa 200
ReplyDeleteWuvu
DeleteNaona simba nao watamfatilia