June 3, 2020


JUNI 7 Yanga itashuka uwanja wa uhuru kukipiga dhidi ya KMC majira ya saa 10:00 jioni ikiwa ni mchezo wa kirafiki.

Mchezo huo utakuwa wa kwanza kwa timu hizo baada ya Serikali kuruhusu masuala ya michezo kuanza baada ya kusimamishwa tangu Machi 17 kutokana na janga la Virusi vya Corona kwa sasa Serikali imeruhusu masuala ya michezo kuanza kwa kueleza kuwa maambukizi yamepungua.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa, Kocha Msaidizi, Charles Mkwassa ameomba mechi hiyo ili kujua ubora wa wachezaji wake.

"Kocha amemba apewe mechi ili kujua ubora wa kikosi chake kwani tunarejea kwenye mechi za ushindani hivyo ni muhimu kuona namna gani kikosi kitakuwa imara," amesema.

Juni 13,Yanga itamenyana na Mwadui FC mchezo utakaochezwa Uwanja wa Kambarage,Shinyanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic