MKURUGENZI wa Uwekezaji ndani ya GSM, Injinia Hersi Said amesema kuwa mpango mkubwa wa kusajili wachezaji ndani ya Klabu ya Yanga kwa sasa ni kutowapa mikataba ya awali nyota wanaowahitaji wakihofia kupigwa bao na watani zao wa jadi Simba.
Injinia amesema kuwa awali walikuwa wakifanya hivyo kwa mastaa ambao walikuwa wanawahitaji mwisho wa siku wanawahiwa njiani kwa kupeleka mikataba yao kwa timu nyingine wakitaka waongezewe dau.
Miongoni mwa wachezaji ambao kwa sasa wapo kwenye rada za Yanga ni pamoja na Heritier Makambo ambaye alikuwa ndani ya Yanga msimu wa 2018/19 kwa sasa anakipiga Horoya.
"Hatuwezi kuwapa mikataba ya awali kwa sasa nyota ambao tunawahitaji kwa kuwa ni imekuwa ikiwapa faida wengine ambapo walikuwa wanapeleka mikataba hiyo kwa timu nyingine ili wapewe dau nono hilo hatutafanya kwa Makambo, tunaongea naye ila mkataba wa awali hatapewa," amesema.
Inaelezwa kuwa Simba wameanza kutazama mienendo ya Yanga ili waipige bao kwa nyota huyo ambaye alijenga urafiki na nyavu kwa kutupia mabao 19.
No sense
ReplyDeleteDalili ya kushindwa. Pochi limeanza kupungua. Kama mna nia na mchezaji na mnadai pesa mnayo tatizo nini?
ReplyDeleteYanakuhusu nini ya Jangwani?
DeleteTatizo jangwani kila mkiongea sentensi moja ya pili mnamtaja simba
Deletepambanani na hali yenu.kazi kutangaza unaoa wakati hata posa hujatoa mdomo unawaponza. hivi hata ligi bado kwisha kila kona makelele yenu. umesikia viongozi wa simba wakiongelea usajili mpya kwa kutaja majina ni ulimbukeni mtupu pale utopoloni hakuna weredi kila mtu ni msemaji wa timu wengine mpaka wanapiga magoti kuomba msamaha wakibanwa baada ya kungea pupu.Timu kila mtu ni msemaji mpaka wachezaji nao wanapendekeza usajili hapo kunatimu au kundi la komedi. umeshawahi kuskia lini Kagere amesema nitawaletea simba mchezaji kutoka Rwanda au Chama aseme ataleta mchezaji kutoka Zambia.wale jamaandoo maana walaitwa Vyura ukienda bwawani kila chura anataka kusikika yeye sasa wanatofauti gani na chura?
Haina mantiki. Sijaona dalili zozote za Simba kumuwania Makambo. Nitashangaa sana kama kweli Yanga wanamtaka Makambo eti washindwe kumpata kwasababu ya Simba. Makambo ni mzuri lakini sio chaguo la Simba.
ReplyDeletepesa ya kuvunja mkataba uliobaki wa miaka 2 pale Horoya imekuwa ni kubwa hawawezi kuna haja gani ya kuzungumza uongo na kuitaja simba kwenye kila jambo mnalofeli . imefika mahali mashabiki yanga wakatae kudanganywa kama watoto kwa kuwaamunisha eti simba wanawaharibia simba hatuwezi kusajili kila mchezaji.hii ndio story ya kudanganyana na kuficha uhalisia wa timu yàko kwa kuambiwa bingwa anabebwa na shabiki unaamini wakati timu iko choka mbaya ina magoli 10 ya kufunga na imefungwa goli 9. akili au matope.
ReplyDeleteYanga bhan!!
ReplyDeleteYani 🐸🐸ni kelele tu mwanzo mwisho
ReplyDeletePovu lawatoka sana mikia kisa kauli ya mwandishi. Zakuambiwa changanya na zako,mwandishi anatafuta ugali kupitia chombo chake lakin sio kila habari ina habari.We shabiki wa mkia umeshawahi fanya usajili hata kwenye timu yako ya mtaani ukajua ni hujuma gan ushawahi fanyiwa!!!? Wacha chombo cha habari kifanye kaz yake kisha tuone mwisho inakuaje. Mbona zikiandikwa habar za mikia hamtoi povu. Duuh!! Kweli nyan haoni ku........!!
ReplyDeleteThe teh teh vyuraaaa
ReplyDeleteThe teh teh vyuraaaa
ReplyDeleteUtopolo FC mbona mnatapatapa sana? Wanachofanya Simba hivi sasa ni kujipanga kumalizia msimu wa VPL na kujihakikishia ubingwa. Msiwapakazie, wala hawajaanza usajili wa wachezaji. Nyie Gongowazi vipi?
ReplyDelete