NYOTA wa Yanga, Mapinduzi Balama huenda asionekane tena uwanjani hadi msimu huu unamalizika kutokana na jeraha lake la kifundo cha mguu linalomsumbua.
Balama alipata majeraha hayo ambapo amevunjika hivi karibuni akiwa mazoezini walipokuwa wanajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ndanda.
Akizungumza na Spoti Xtra, Daktari wa Yanga, Shecky Mngazija, amesema jeraha alilonalo Balama linahitaji muda zaidi ili awe sawa ambapo anatakiwa kukaa kwa takribani siku 14 ndipo mfupa uanze kuunga.
“Kwa kawaida mfupa wa binaadamu ukivunjika unaanza kuunga ndani ya siku 14 na kuanzia wiki sita hadi nane ndio unakamilika kwa kutegemea na majeraha aliyoyapata muhusika.
“Kuunga kwa haraka kunategemea pia chakula kizuri atakachokula, mapumziko ya kutosha pamoja na dawa atakazopewa.
“Balama anaendelea na matibabu, kuna vifaa ambavyo vinatumiwa kwa ajili ya kuunga mguu, kwa sasa yupo kambini kwa kuwa wenzake wote wapo kambini na tukimruhusu kurudi nyumbani atakosa wa kumuhudumia, hivyo bora abaki hapa,” alisema Mngazija.
Zimebaki takribani wiki tatu kumalizika kwa msimu huu wa Ligi Kuu Bara, hivyo Balama hadi akija kupona, msimu utakuwa umemalizika.
M7ngu ampe wepesi wa kupona haraka arudi kazini
ReplyDeleteKila la Heri balama.
ReplyDelete