July 6, 2020


SHOMARI Kapombe, beki wa kulia wa Klabu ya Simba inaelezwa kuwa kuna hatihati ya kukosa mechi zote za Simba msimu huu kutokana na majeraha ya mguu aliyopata.


Kapombe aliumia mguu Julai Mosi Uwanja wa Taifa baada ya kuchezewa rafu na Frank Domayo nyota wa Azam FC.

Kwenye mchezo huo, wa hatua ya robo fainali Simba ilishinda mabao 2-0 watupiaji wakiwa ni John Bocco na Clatous Chama. 

Simba itakutana na Yanga Julai 12 Uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa nusu fainali inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa Kapombe ataukosa pia mchezo huo. 

Mshindi wa mchezo huo atakutana na mshindi wa mchezo kati ya Sahare All Stars na Namungo FC utakaochezwa Uwanja wa Mkwakwani.

Simba Julai 8 itamenyana na Namungo Kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambapo watakabidhiwa kombe lao.

Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa wachezaji wote wa Simba wapo kambini isipokuwa Kapombe ambaye anaendelea kupewa matibabu. 
Kapombe ana jumla ya asisti saba ambapo ametoa sita Kwenye ligi na moja Kwenye Kombe la Shirikisho.

13 COMMENTS:

  1. Huyu domayo aache ushetani wake. Sasa anajisikia raha gani kuwaumiza wenzake? Alimwiimiza Boko akakaa njee miezi minne. Na huyu naye kamtoa nje miezi minne. Mpira ni kazi na ndio inalisha wachezaji aache upuuzi wake.

    ReplyDelete
  2. Huyu inabidi naye aumizwe akae nje msimu mzima anatafuta sifa zisizo na maana

    ReplyDelete
  3. Karma never misses an adress. Domayo atapata haki yake.Ni suala la muda tu.

    ReplyDelete
  4. Nimesikitishwa zaidi na kitenda cha Domoyo, hakiki sijui tatizo ni nini jamani.

    ReplyDelete
  5. Mpira ni mchezo wa kuwakutanisha watu kwa kujuana na upendo na sio kumtendea ndugu yako uadui wa kumkatia ndugu maisha na kumsabibishia madhara pia aila yake nzima inayomtegemea. Tulishuhudia kuwa alimfanyia makusudi kwa nia ya kumuangamiza na sasa anasema sijakususudia. Huyu si mchezaji Bali ni adui ambaye anastahaki adhabu ili pia iwe funzo kwa maadui wengine. Huyo ni lazima asimamishwe kucheza na pia kuhudhuria mpira kwa muda usiopunguwa mwaka na kulipishwa gharama isiyopunguwa shilingi milioni moja

    ReplyDelete
  6. Domayo agharamie pia matibabu ya Kapombe ili ajue kitendo alichofanya hakikubaliki. Yote kwa yote Mungu Muweza atamwangazia Kapombe uponaji wa haraka.

    ReplyDelete
  7. Frank Domayo anajifunza nini kupitia maoni ya watu? Kwa kweli Mungu "anamuona" kwani maskini Kapombe hana muda mrefu tangu arejee kwenye kucheza baada ya kukaa nje kwa muda mrefu akiteseka kuuguza majeraha. Shukrani uongozi wa Simba ulimpambania sana

    ReplyDelete
  8. Huyo Domayo katumwa Kama hajatumwa akapimwe akili, Ni mpumbavu anaukatili usiyonamaana analigharimu taifa kwakukosa akili.

    ReplyDelete
  9. Acheni unazi wenu huo kwenye mpira kumia ni jambo la kawaida tunaona uko majuu watu wanavunjika miguu sàsa kumia kwa kapombe imekuwa tatizo

    ReplyDelete
    Replies
    1. sio tatizo kama ilivyo kwa Niyonzima na Mapinduzi...Simba ina kikosi kipana.. Kukosekana kwa Bocco kulipunguza magoli lakini sio ushindi wa timu ya Simba..

      Kukosekana Niyonzima na Mapinduzi hakuiiathiri chocote Yanga

      Delete
    2. Ukitoa comments uwe na huruma kwa aliyeumizwa tena kwa makusudi. Unasupport vitendo vya Domoayo inaelekea. Sasa huo unazi wako ni wa kupitiliza na hasa ni wa kiwango cha juu sana. Ni mtu gani wewe unayependezwa na kuumizwa kwa binadamu mwenzako tena kwa mchezaji tu kujiona yeye ni kisirani wa kuwaumiza wenzake?

      Delete
  10. Tatizo sio kuumia kwa kapombe, ni namna alivyoumizwa, na jinsi domayo anavyowaumiza wengine. Kumbuka alimwuumiza Boko amekaa nje ya uwanja miezi 4. Hata huko ulaya wachezaji wa aina hii wapo ndio na wanalalamikiwa pia. Mtu kama Ramos hujasikia anavylaniwaga? Kuvunja mtu mguu sio sifa, ni ushetani, na hasa kama ni rafu ya maksudi kama anazocheza rafiki yako domayo.

    ReplyDelete
  11. Kumbe ndiye aliyemuumiza Bocco pia? Huyo ana ushetani ndani yake. Achunguzwe vizuri.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic