UONGOZI wa Simba unavutana na kiungo wa Yanga, Mkongomani, Papy Tshishimbi, anayetaka dau la usajili la dola 50,000 (zaidi ya Sh mil 115) na mshahara wa Sh milioni 10 kwa mwezi asaini mkataba wa kukipiga Msimbazi, lakini wakati wakivutana upande wa pili Yanga nao wanakaribia kumsainisha mkataba mpya.
Kiungo huyo ambaye pia anamudu kucheza nafasi ya kiungo mshambuliaji, ni kati ya wachezaji wanaotajwa kujiunga na Simba kwenye msimu ujao kwa ajili ya kuiimarisha safu ya kiungo inayochezwa na Jonas Mkude, Mzamiru Yassin na Mbrazili, Gerson Fraga.
Mkongomani huyo hivi sasa anaruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu nyingine itakayomuhitaji kutokana na mkataba wake wa miaka miwili kumalizika mwishoni mwa msimu huu.
Taarifa zinaeleza kuwa mbali na dau hilo la usajili, kiungo huyo ameomba mshahara wa Sh milioni 10 kwa mwezi na usafiri wa gari aina Toyota Athlete Crown atakalotumia kwenye mizunguko yake binafsi kwa kipindi chote akiwa anaichezea Simba kwa muda wa miaka miwili.
Aliongeza kuwa baada ya kiungo huyo kutaja ofa hizo, uongozi wa Simba umeonekana kutokubaliana naye kwa kumuomba apunguze kiwango hicho cha fedha ya usajili huku wakimuahidi kumpatia mshahara na gari hilo analolihitaji.
“Simba wameonekana kukaa kimya ikiwa ni siku chache tangu Tshishimbi alipowapa ofa viongozi wa timu hiyo waliyoomba kwa ajili ya kuipeleka kwenye Bodi ya Wakurugenzi ya Simba iliyo chini ya bilionea kijana, Mohamed Dewji ‘Mo’.
“Ofa hiyo imeonekana ni kubwa kutokana na kuhitaji kiwango kikubwa cha fedha ambacho ni Sh mil 115, mshahara wa Sh Mil 10 na gari binafsi.
“Hivyo, viongozi hivi sasa wanajadiliana na kama mambo yakienda vizuri, watafikia muafaka mzuri wa kusaini mkataba Simba, lakini uongozi wa Yanga nao upo kwenye mazungumzo mazuri na kiungo huyo anayeonekana anaangalia maslahi katika klabu hizi mbili,” alisema mtoa taarifa huyo.
Jamani huyu Tshishimbi si alishamalizana na Hersi Said wa GSM?
ReplyDeleteZile zilikuwa mbwembwe za Injinia tu katika kuwatuliza washabiki wa Yanga. Lakini Tshishimbi na Morisson bado ni 'pasua vichwa' Yanga
DeleteNdio waandishi wetu wanaandika kwa mapenzi ya timu zao
DeleteNa Tshishimbi hajaonekana uwanjani tangu ligi irejee. Au ndiyo hizo danganya watu kuwa ana majeraha?
ReplyDeleteHuyu anajipandisha thamani kwa kuotimia Simba ili yanga wampe donge nono. Hana hiyo thamani
ReplyDeleteKila siku habari Tshishimbi na Morisson tu, hebu andikeni na za wachezaji wengine kina Boxer, Jaffar na Raphael Daud...
ReplyDeleteNaunga mkono hoja. Waandike pia habari za vilabu vingine vya Tanzania. Kwani viko viwili tu Yanga na Simba?
Delete