July 28, 2020


SHIRIKISHO la Soka la nchini Afrika Kusini (SAFA) limemfutia jumla vibali vya kazi Luc Eymael aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga kufanya kazi ndani ya nchi hiyo.

Eymael Julai 26 baada ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Lipuli alisambaza taarifa ambazo zilikuwa zinaonyesha ubaguzi wa rangi na kusema watanzania hawajui soka.

Mchezo huo Yanga ilishinda bao 1-0 lililofungwa na David Molinga ambaye amefikisha mabao 11 ndani ya Ligi.

Tayari Yanga imeshamfuta kazi Eymael jumla kutokana na kitendo hicho na kuomba radhi kwa mashabiki, Serikali na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF).

Kocha huyo pia aliomba msamaha kwa kueleza kuwa alifanya hivyo kutokana na hasira alizokuwa nazo kwa kupitia kipindi kigumu ndani ya Yanga.

3 COMMENTS:

  1. Mwandishi hujaeleza sababu za Afrika kusini kumfutia leseni. Jee ni hizi hizi za yanga/ Tanzania au na huko alifanya kosa fulani?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sababu ni hizihizi, nimesoma taarifa ya SAFA. Pia nao wanampango wa kureport issue hiyo FIFA

      Delete
  2. Duh! Kweli kufa kwa nyani, miti yote huteleza

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic