October 13, 2017




Wachezaji wa klabu ya Simba SC wamepata nafasi ya kutembelea ofisi za kampuni ya SportPesa ambao na wadhamini wakuu wa mabingwa hao mara 18 wa Ligi Kuu ya Tanzania bara pamoja na kombe la Shirikisho.

Wachezaji wa Simba wakiongozwa na nahodha Method Mwanjale pamoja na uongozi mkuu wa klabu hiyo akiwemo Afisa Habari, Haji Manara, uliwasili ofisini hapo majira ya 10:00 kamili jioni ambapo walipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa SportPesa, Pavel Slavkov pamoja na Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji,Tarimba Abbas.


Moja ya mambo ambayo yalikuwa ni mada ya kuu ya mazungumzo ni pamoja na uhusiano kati ya klabu hiyo ambao ni mabingwa watetezu wa kombe la Shirikisho pamoja na SportPesa ambapo taasisi hizo mbili zimeingia mkataba wa miaka mitano wa udhamini mwezi Mei mwaka huu.

Sambamba na mahusiano ya taasisi hizo mbili, lakini wachezaji wa Simba walipata fursa ya kumegewa somo juu ya masuala ya teknolojia ikiwa ni pamoja na matumizi ya kurasa zao za mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter na Instagram, somo ambalo lilitolewa na Kelvin Twissa, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa SportPesa.
Thamani ya Mchezaji
Sambamba na matumizi ya teknolojia na umuhimu wake kwa wachezaji, nyota hao wa Simba walipewa maneno mawili matatu kuhusiana na vitu vinavyopelekea thamani ya mchezaji kuongezeka, somo ambalo lilitolewa na Bwana Tarimba Abbas, Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa.
“SportPesa ni kampuni inayojulikana kimataifa na Simba ni klabu kubwa inayojulikana Tanzania na Afrika, kwahiyo unapokuwa mchezaji wa klabu ya Simba ni lazima uwe mtu ghali.
“Suala kubwa linalokuja hapa ni wewe mchezaji unajifanya ghali kiasi sana lakini ni lazima ujue kuwa ughali wako unakuja sambamba na uwezo wako uwanjani.
“Sio unakuwa mtu unayeonekana mara kwa mara vijiweni, kila siku unazungumza wewe. Fanya kazi uwanjani, acha watu wakuzungumzie wewe’, alisema Bwana Tarimba.
Baada ya somo hilo murua, uongozi wa Simba ulitoa shukrani zake za dhati kwa wadhamini wao, SportPesa kwa kukabidhi cheti maalum sambamba na jezi ambayo ilisainiwa na wachezaji wote wa Simba.
Baada ya zoezi hilo, wachezaji wa Simba walishindana kupiga danadana na wafanyakazi wa SportPesa ambapo kwa upande wa Simba, kiungo Mzamiru Yassin pamoja na Erasto Nyoni waliongoza mashambulizi na baada ya hapo uongozi wa pande zote mbili pamoja na wachezaji walipiga picha ya pamoja.

Hii ni mara ya kwanza kwa klabu ya Simba kufanya ziara kwa wadhamini wao SportPesa, tangu waliposaini mkataba wa udhamini mwezi Mei mwaka huu, kitendo ambacho kinadumisha uhusiano wa pande zote mbili sambamba na kubadilishana mawazo. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic