July 2, 2020


WADAU wa michezo wamempa neno nyota wa Klabu ya Azam FC, Frank Domayo kwa kumtaka aendelee kwenye asili yake ya kucheza soka la umakini kwa kuwa sio kawaida yake kucheza rafu ndani ya uwanja.

Kwenye mchezo uliochezwa jana, Julai Mosi mbele ya Simba, Azam FC ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 ambapo Domayo alionekana akimchezea rafu beki wa Simba Shomari Kapombe.

Leo Kapombe anatarajiwa kufanyiwa vipimo ili kujua ukubwa wa tatizo lake kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandnbroeck.

Kilanga Mselemu amesema kuwa soka sio vita hivyo ni lazima kuwa na umakini katika vitu ambavyo wanafanya wachezaji ndani ya uwanja na sio kutegemea kuomba radhi.

Melak Kapinga amesema kuwa Domayo ni mchezaji mzuri na jambo ambalo amelifanya jana sio kawaida yake anadhani inatokana na jazba ya mpira wa jana hivyo lazima asamehewe ili mambo yazidi kusonga mbele.

 Ushindi wa Simba unaipa tiketi ya kucheza hatua ya nusu fainali ambayo inatarajiwa kuchezwa mwezi huu Julai.

13 COMMENTS:

  1. Alishawahi kufanyiwa na Mkude mechi ya Simba na Yanga,pia alishawahi kukanyagwa tumboni na MO IBRAHIM Mechi ya Azam na Simba.Yote hayo hamkuyaona ila leo kugusa katimu chenu cha kipumbavu mnalaumu.Mbaona yule babu WAWA na mwenzake CHAMA walipowakanyaga kwa makusudi wachezaji wa YANGA hakuna rahi mliyoitoa?Acheni umbumbumbu nyie mpira ni wa wote sio MIKIA tuu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyo mbwa wenu Domayo c ndo aliyefanya Boko akakaa benchi kwa muda mrefu halafu mnasema bahati mbaya ya nini wakati ni dhamira yake...kwani peke yake alikuwa na temper mchezon...refa alimbeba tu kwani alicheza rafu zaidi ya moja

      Delete
  2. Lazima wachezaji wakubwa na wa timu kubwa walindwe kwa garama yoyote wachezaji wa simba wanatarajiwa kucheza ligi ya mabingwa uwezi fananisha na utopolo ambao hawana majukumu ya kitaifa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa ustaarabu wa dunia ya kisasa mchezaji yoyote anatakiwa kulindwa. Michezo ya kibabe, na kihuni haitakiwi kuvumilwa hata kidogo. Mawazo yako ni ya kishezi! Upeo wako wa kuelewa mambo ni ziro kabisa! Unatia kinyaa! Ndio tatizo la kuchanganya mataputatapu, gongo na bangi!

      Delete
  3. Unahitaji msaada wa kitaalamu. Mimi ni Yanga lakini sikubaliani na logic yako.Kosa likifanywa haijalishi kafanya nani na kafanyiwa nani. Two wrongs does not make it right.

    ReplyDelete
  4. Kapombe juzujuzi wamemuomba achezee timu ya taifa halafu kachezaji ambacho hakana hata umuhimu kanamuumiza

    ReplyDelete
  5. Kapombe siyo muungwana. Huwezi kujifanya umeumia kwa kuguswa kidogo tu. Anataka watu wamuone Domayo mbaya.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Domayo ndiye aliyemuumiza John Bocco na kusababisha akawa nje ya soka kwaajili ya matibabu ...msimtetee huyo anavuta bangi

      Delete
    2. Kuguswa kidogo? Mbona domayo mwenyewe anakiri kumuumiza Kapombe? Acha kuona jambo hilo kuwa zuri tukemee mambo ya kuumizana kwa kusudi iwe Simba iwe Yanga iwe Azam iwe timu nyingine yeyote sio vizuri kuumizana wachezaji.

      Delete
  6. Enter your comment...hili la domayo halipaswi kufumbiwa macho kwasababu ameanza kuzoea hiyo tabia ya kuumiza wenzake,alimchezea Bocco rafu mbaya kwenye mechi ya ngao ya hisani akakaa benchi karibu mechi zote za mzunguko wa kwanza,huyu anawafahamu vizuri hao kwahyo anajua aguse wapi awaweke benchi

    ReplyDelete
  7. Mi nadhani angejaribu na wachezaji wa Utopolo ndo wana uvumilivu Sisi Simba hatuwezi kuvumilia ujinga wa aina hii...kwani ameshazowea ...

    ReplyDelete
  8. Domayo anaonekana kuwa anadhamiria kuwaumiza wenzake. Sasa hiyo sio sawa apewe adhabu ya kumlumbusha kuwa mpira sio ugomvi

    ReplyDelete
  9. Domayo hana hutu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic