Yanga imetua salama mjini
Tunis na sasa imeanza safari kwenda mjini Sousse, umbali wa takribani saa mbili
kwa basi.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga,
Clement Sanga ndiyo ameongoza msafara huo.
Pamoja naye, kuna wadau
kadhaa akiwemo kiungo wa timu ya Gymkhana, Mudy Sebene pamoja na Maulidi
Kitenge ambaye ni mtangazaji wa EFM Radio pamoja mchambuzi wa michezo wa gazeti
la michezo la Championi.
Yanga inatarajia kutua
Sousse leo jioni, baada ya hapo itaanza maandalizi ya mechi hiyo ya keshokutwa
dhidi ya Etoile du Sahel.
Mechi ya kwanza jijini Dar,
timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.
KAKA nahitji kupata msaada wako jins ya kuendeshablog yangu ayububida.com
ReplyDelete