BERNARD Morrison, kiungo mshambuliaji wa Yanga, amesema kuwa anamuomba Kocha Mkuu, Luc Eymael ampange kwenye mchezo huo ili afanya kazi yake mbele ya Simba.
Yanga itamenyana na Simba, kesho Julai 12 Uwanja wa Taifa majira ya saa 11:00 jioni kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho.
Morrison alikuwa na mvutano wa kimkataba na masuala ya nidhamu na baadhi ya viongozi wa klabu yake ila kwa sasa amesharejea kambini na alikuwa kwenye kikosi kilichoshinda bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa ligi.
Morrison amesema: “Nikipata nafasi ya kucheza nitaendelea kulinda heshima yangu na ya klabu, muhimu naomba Mungu niwe na afya njema kisha kocha anipe nafasi ya kucheza.
“Ninachohitaji ni sapoti ya mashabiki ambao wamekuwa wakiniunga mkono tangu nimefika hapa Tanzania, kama timu tunataka kuendelea pale tulipoishia.
“Tunahitaji matokeo mazuri ili kupata nafasi ya kucheza michuano ya kimataifa msimu ujao, muhimu naomba kocha anipe nafasi kama nitakuwa fiti kiafya kisha mashabiki watuunge mkono katika mchezo huo muhimu."
Hivi yanga wana mchezaji mmoja tuu? Au kwa vile yeye ndio mbeba tunguli?
ReplyDeleteWaandishi viazi
DeleteWangemwandika kagere au mama yako usingesema yote hayo
ReplyDeleteKuwa na heshima kijana hapa hatuzungumzii familia
DeleteTshishimbi ameacha pengo kubwa kwenye midfield. Mechi itategemea Simba wanaingia na approach gani. Yanga kama kawaida wataanza kukabia juu wasiruhusu Simba wasichezee mpira hata kidogo. Sven analijua hilo kazi kwake.
ReplyDeleteUnatumia jicho gani kuona mambo makubwa kiasi hicho?it is more than 3rd eye,una vission kubwa sana na kesho kazi inaweza ikawa nyepesi sana kwa simba kuimaliza Yanga,but lets wait and see,THE TIME WILL TELL.
DeleteHumu hatutaki lugha za kuudhi, nashangaa meenye blog kakaa kimya watu wanatukana bila staha
ReplyDeleteNakuunga mkono
Delete