MBALI na kujenga urafiki na nyavu mshambuliaji namba moja wa Simba, Meddie Kagere raia wa Rwanda anapenda kusoma vitabu kuhusu mafanikio.
Kwenye Ligi Kuu Bara metupia mabao 19 na pasi tano za mabao ndani ya Simba ambayo imefunga jumla ya mabao 69.
Ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 80 Simba imebakisha mechi tano kukamikisha mzunguko wa pili ndani ya msimu wa 2019/20.
Tayari shughuli ya ubingwa wamemaliza kwa kuwa walipolazimisha sare mbele ya Tanzania Prisons walishakamilisha kabisa zoezi la kutwaa ubingwa kwa kufikisha pointi 79 ambazo hazitafikiwa na timu nyingine.
Kwa sasa imebaki vita ya nafasi ya pili ambayo Yanga na Azam wanapambania Kombe huku Kagere akiwa na kazi ya kufikia rekodi yake aliyoweka msimu wa 2018/19 ya kufunga mabao 23.
Anavutwa shati na mzawa Yusuph Mhilu wa Kagera Sugar mwenye mabao 13 na Obrey Chirwa wa Azam FC mwenye mabao 12.
Julai 8 watakabidhiwa Kombe lao watakapomalizana na Namungo FC Uwanja wa Majaliwa,Lindi.
Kagere ajitathimini, uwezo wake unashuka kwa kasi ya 4G
ReplyDelete