July 12, 2020


ADAM Oseja, kipa namba mbili wa Namungo amesema kuwa ni ngumu kwa timu pinzani kusepa na pointi tatu Uwanja wa Majaliwa kwa kuwa wamejijengea ngome ya kujiamini zaidi wanapokuwa na mashabiki wao.
Julai 8 wakati Simba inakabidhiwa rasmi ubingwa wao wa tatu mfululizo walibanwa mbavu na Namungo kwa kulazimisha sare ya bila kufungana na kuwafanya wagawane wote pointi mojamoja.
Akizungumza na Saleh Jembe, Oseja ambaye aliipandisha Namungo kutoka Ligi Daraja la Kwanza msimu wa 2019/20 alisema kuwa kasi ya wachezaji ndani ya Uwanja wa Majaliwa huwa tofauti wakiwa nje.
“Majaliwa pale sio sehemu salama kwa wapinzani kwani ni timu moja tu ambayo ni Coastal Union waliweza kuondoka na pointi tatu ila wengine wanapata tabu kupata pointi tatu kwa kuwa wanakutana na balaa zito uwanjani.
“Kinachotubeba ni ushirikiano pamoja na nguvu ya mashabiki ambao wanatupa sapoti, ushirikiano mkubwa kwa kila mmoja inatufanya tunakuwa bora,” amesema.
Namungo ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 60 baada ya kucheza mechi 34, imefungwa mabao 30 na safu yake ya ushambuliaji imefunga mabao 42.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic