July 12, 2020


KALIDOU Koulibaly, nyota anayekipiga ndani ya Klabu ya Napoli amesema kuwa hana mpango wa kutimka ndani ya timu hiyo kwa sasa na anatamani kumalizia maisha yake ya soka hapo.

Beki huyo amekuwa akitajwa kuibukia ndani ya Klabu za Manchester City pamoja na United ambao wote inaripotiwa kuwa walikuwa wanahitaji saini yake.

Pia Mabingwa wa Ligi Kuu England, Liverpool nao wanatajwa kuingia kwenye rada za kuwania saini ya beki huyo pamoja na Barcelona na PSG zote zinatajwa kumtazama beki huyo.

Ripoti zinaeleza kuwa beki huyo anatamani kuendelea kubaki ndani ya kikosi hicho kutokana na ushirikiano anaopata kutoka kwa wenzake.

Koulibaly amesema:"Sijazungumza na Napoli kuhusu kuondoka kwangu ndani ya klabu kwa sasa kuhusu kuondoka, sijazungumza kabisa kuhusu hilo ila nimesoma tu kwenye magazeti ninapenda kubaki hapa ."

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic