July 7, 2020


IMEELEZWA kuwa sababu sababu kubwa ya kiungo wa mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison kuwahi kwenda ndani ya kikosi hicho ni kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba.

Simba itamenyana na Yanga, Julai 12 Uwanja wa Taifa mchezo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili.

Morrison, alibaki Dar wakati Yanga ikimenyana na Biashara United ya Mara, Julai 5 kwenye mchezo uliokamilika kwa sare ya bila kufungana Uwanja wa Karume.

Jana, Morrison alikwea pipa kujiunga na Yanga Bukoba kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa kesho, Julai 8 dhidi ya Kagera Sugar.

Kocha wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa uhitaji wake kwenye kikosi ni kushinda na Morrison alimwambia kuwa yupo tayari kucheza.

"Morrison yupo tayari kucheza na nina amini kuwa ataendelea kutumika ndani ya Yanga," amesema.

Kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Machi 8, Uwanja wa Taifa, Morrison alifunga bao pekee la ushindi lililoipa Yanga pointi tatu jambo ambalo limemfanya  Eymael amuwahishe kambini ili awe fiti.

3 COMMENTS:

  1. Sisi tunasema Yanga ni kubwa kuliko Morrison, lakini mbona Morrison antuinjoy anavotaka mwenyewe nasi mikono juu kwahivo anajiona tunamuabudu na yupo huru na Kuna hatari wengine wakaiga nyayo zake

    ReplyDelete
  2. Ukisoma alama za nyakati utaelewa tu

    ReplyDelete
  3. Morrison na Niyonzima ndio ma superstars wa Yanga kwa sasa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic