July 16, 2020


JOHN Bocco nahodha wa Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo dhidi ya Mbao FC utakaopigwa Uwanja wa Taifa.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa majira ya saa 1:00 usiku.Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza Kirumba, Mbao ilikubali kufungwa mabao 2-1.

Simba inakutana na Mbao FC ambayo gari limewaka baada ya kupata ushindi kwenye mechi zake tano mfululizo zilizopita na mchezo wake wa hivi karibuni walishinda bao 1-0 mbele ya Mtibwa Sugar.

Tayari Simba ni Mabingwa hivyo hawana cha kupoteza ila wanakutana na Mbao ambao wanapambana kujinasua kushuka Daraja.

Ipo nafasi ya 19 Mbao FC baada ya kucheza mechi 34 na kibindoni ina pointi 35 huku Simba ikiwa kileleni na pointi 81.

Bocco amesema:"Wapinzani wetu ni timu nzuri hilo tunalitambua ila sisi tunahitaji kuongeza pointi zaidi baada ya kuchukua ubingwa na tumeshajiandaa vema, mashabiki watupe sapoti."

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic