OWEN Chaima, kipa namba moja wa Singida United amesema kuwa hatakuwa na timu hiyo Ligi Daraja la Kwanza kwa kuwa anaamini katika uwezo wake akiwa langoni.
Chaima ambaye aliwahi kukipiga pia ndani ya Mbeya City ameongeza kuwa hana mkataba na timu hiyo jambo linalomfanya asijue kuhusu kesho yake.
Kipa huyo jana, Julai 15 alikaa langoni wakati timu yake ikikubali kichapo cha mabao 3-1 mbele ya Yanga, Uwanja wa Taifa.
"Nina uwezo mkubwa hilo lipo wazi kwani mashabiki wanajua kwamba nilikuwa Mbeya City na nilitoka na clean sheet nyingi tofauti na hapa Singida United mambo yamekuwa magumu.
"Kikubwa ni maandalizi tu kwani kuna mechi nyingine tulikuwa tunafungwa mabao mengi hiyo ilikuwa inatuumiza ninasema nikipata timu nyingine hapa Bongo nitafanya makubwa zaidi," amesema Chaima maarufu kama Handsome Boy.
0 COMMENTS:
Post a Comment